Baada ya Tundu Lissu, Mritaba Kupigwa Risasi, Mkuu Wa Majeshi Afunguka…
MKUU wa
Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Venance Mabeyo, amezungumzia matukio ya kiuhalifu kwa
watu kupigwa risasi yanayoendelea Tanzania, akisema vyombo vya ulinzi vipo
kazini na hivi karibuni hali itakuwa shwari.
Akizungumza katika
mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam Jumatano Jenerali Mabeyo
alionyesha kushangazwa na matukio ya sasa kuonyesha kushtua watu wengi, tofauti
ya yaliyotokea Kibiti mkoani Pwani, yaliyoua zaidi ya watu 35.
“Kwa nini matukio yaliyotokea Kibiti hayaleti mshtuko mkubwa
wakati watu walioathirika Kibiti ni wengi zaidi kuliko matukio ya sasa, mimi
sitaki kuingia huko,” alisema.
Alisema kwa matukio ya sasa ya kupiga watu kwa risasi,
uzoefu unaonyesha wanaoyatekeleza ni watu ambao hawajapitia kwenye Jeshi la
Kujenga Taifa (JKT).
“Vijana wanaohusika katika uhalifu hawajapitia Jeshi la
Kujenga Taifa, kwa hiyo tuna imani kabisa vijana wetu wanaopitia Jeshi la
Kujenga Taifa wanakuwa na maadili, wanakuwa na nidhamu, nitaomba ninyi
mtusaidie katika wale watakaokuwa wamekamatwa katika kuwahoji, tuone kama
watakuwa wamepitia Jeshi la Kujenga Taifa,” alisema Jenerali Mabeyo.
Kauli hii imetolewa na Jeshi baada ya matukio makubwa ya
watu kupigwa risasi yaliyotokea nchini hivi karibuni, ni pamoja na lile la
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, aliyepigwa risasi Septemba 7 mjini
Dodoma na watu wasiojulikana.
Jingine ni lile la Jenerali mstaafu, Vincent Mritaba,
aliyepigwa risasi na watu wanaosadikika kuwa ni majambazi wakati akiingia
nyumbani kwake Ununio wilayani Kinondoni jijini Dar es Salaam akitoka benki
siku tatu zilizopita.
Lissu kwa sasa yupo Nairobi nchini Kenya akiendelea na
matibabu, huku hali yake ikielezwa kubadilika badilika wakati Jenerali Mritaba,
anatibiwa katika Hospitali ya Jeshi Lugalo, Dar es Salaam na afya yake
inaelezwa kuimarika
Jenerali Mabeyo alisema kuwa vyombo vya ulinzi na usalama
vinashughulika na matukio kadiri yanavyojitokeza na anaamini hali itakuwa
shwari.
“Matukio yanayoendelea tunakabiliana nayo, vyombo vya ulinzi
na usalama wakati wote vinakabiliana na matukio kadiri yanavyojitokeza,
Ninaamini hali itakuwa shwari na sasa vinashughulika.
“Hoja ya msingi tunataka kujiridhisha silaha hizi zinatoka
wapi, hawa watu ni wa aina gani. Sasa vyombo mviachie vifanye kazi yake, msitoe
majibu haraka, tukio linapotokea lazima uangalie limetokeaje, chanzo ni nini, au
sababu ni nini,” alisema Jenerali Mabeyo.
[1.00 MB]NOMA SANA, KuDOWNLOAD VIDEO YaO WAKIBANDUANA BONYEZA HAPA CHINI==>>
0 comments: